LEWIS HAMILTON ASHINDA BAHRAIN GRAND PRIX, TEAM FERRARI MAJANGA YAWARUDISHA NYUMA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 1, 2019

LEWIS HAMILTON ASHINDA BAHRAIN GRAND PRIX, TEAM FERRARI MAJANGA YAWARUDISHA NYUMA.Wakati jana mida ya jioni mechi kali ya ligi kuu ya England kati ya Liverpool na Tottenham ikiendelea, huku upande mwingine kulikuwa na muendelezo wa ligi ya mbio za magari maarufu kama FORMULA 1. Hii ilifanyika Bahrain. 

Katika mbio hizo, Bingwa mara 5 wa ubingwa wa mbio hizo muingereza Lewis Hamilton kutoka timu ya Marcedes aliibuka mshindi baada ya kumpita vizuri dereva wa Ferrari Charles Lecrec ambaye alianza mbio akiwa katika pole position (nafasi ya kwanza kimpangilio). 

Lewis alimpita Charles katika raundi ya mwisho katika kona ya mwisho na kuwashangaza wengi ambao waliona kuwa Charles alikuwa keshashinda. 

Mpinzani mkubwa wa Hamilton, Sebastian Vettel wa Ferrari alipata matatizo baada ya gari lake kuserereka vibaya na kuacha njia. Hiyo iliruhusu watu wengi wamuache numa ingawa alipigana hadi kumaliza nafasi ya 5. 

Hii ni mara ya kwanza kwa Lewis Hamilton kushinda mbio hizi kwa mwaka 2019 na hizo zilikuwa ni mbio za pili kwa mwaka huu. Za kwanza zilikuwa kule Australia na mchezaji mwenzake wa Marcedes aitwaye Bottas ndiye aliyeshinda. 

Hamilton anakuwa wa pili sasa kwenye msimamo wa ligi hiyo akiwa na pointi 43 huku mwenzake Bottas akiongoza na pointi 44. Michuano hiyo inaelekea China sasa. Je Team Ferrari wataweza kufanya maajabu? au watakubali kuwa wanyonge wa Marcedes? 
Loading...

No comments: