NILIMPENDA, NILIUMIA KUACHANA NA AMIN- LINAH - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 11, 2019

NILIMPENDA, NILIUMIA KUACHANA NA AMIN- LINAH

Staa mrembo wa Bongo Fleva, Linah Sanga amesema kuwa aliumia kuachana na msanii Amin sababu alikuwa anampenda kwa dhati.

Linah Sanga na Amin


Akiongea kenye kipidi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, akiwa atanambulisha wimbo mpya wa 'Nimenasa' aliyoshirikiana na  Amin, Linah alisema

"kiukweli hakuna kitu kinauma kama kuachana na mtu unayempenda, mimi binafsi ninampenda Amini ndiyo maana niliumia".

"Hakuna asiyejua kuwa mimi na Amini tulikuwa wapenzi, kwahiyo watu wanaosema kuwa hivi sasa tumerudiana, hatuwezi kuwazuia kwa sababu wanapenda kutuona jinsi tulivyokuwa tukipendana", Linah  alieleza alipoulizwa kuwa alijisikia vipi alipoachana na Amin.


Kuhusu uhusiano wao kwa sasa, Linah amesema atatafuta wakati rasmi wa kutambulisha penzi lao, lakini kwa sasa watambue tu kuwa wako pamoja na lolote linaweza kutokea.

Picha za ukaribu za wawili hao zilizua mjadala mtandaoni wengi wahisi kuwa wawili hao wamerudisha penzi lao za zamani.


AMIN ATOBOA KUHUSU YEYE NA LINAH
Loading...

No comments: