London Marathon 2019: Eliud Kipchoge ashinda London Marathon mara ya nne mfulululizo - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, April 28, 2019

London Marathon 2019: Eliud Kipchoge ashinda London Marathon mara ya nne mfulululizo


Mkenya Eliud Kipchoge ashinda London Marathon 2019PA
Mkenya Eliud Kipchoge
Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda London Marathon kwa mara ya nne mfululizo.
Kipchoge, 34, ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mbio hizo mjini Berlin mwaka jana, alikamilisha mbio za leo kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thalathini na nane (2: 02: 38.)
Waethiopia Mosinet Geremew na Mule Wasihun walimaliza katika nafasi ya pili na ya tatu nyuma ya Kipchoge, ambaye alikosa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya Dunia kwa sekunde 59 ambayo ilikua 2:01:39. 
Muingereza Mo Farah alichukua nafasi ya tano baada ya kumaliza dakika 3 na sekunde moja nyuma ya Kipchoge, huku Muingereza Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya 10.
Mkenya mwingine Brigid Kosgei, 25, alishinda mbio hizo upande wa kinadada na kuwa mwanamke wa kwanza wa umri mdogo kushinda London marathon upande wa wanawake.
Kosgei alimshinda bingwa mtetezi Vivian Cheruiyot kwa kutumia mda wa saa 2:18:20 kushinda mbio hizo kwa mara ya kwanza.
Mkenya Vivian Cheruiyot alichukua nafasi ya pili huku Roza Dereje wa Ethiopia akimaliza wa tatu.
Muingereza Charlotte Purdue alimaliza nafasi ya 10.


Ukweli kuhusu mbio za London Marathon
  • Watu 444,168 wamejiandikisha kuchangia mbio za mwaka huu idadi ambayo ni zaidi 7.3% ikilinganishwa na mwaka jana.
  • 44% ya watu waliyotoa maombi ya kishiriki mbio hizo ni wanawake na nusu ya wakimbiaji hawajawahi kushiriki mbio za marathon.
  • Waandaaji wa mbio hizo mwaka huu wanalenga kukusanya jumla ya pauni milioni 3.5
  • Kundi la wanaume linalojiita ''Ever Presents'' limekua likishiriki mbio hizo tangu mwaka 1981SOMA ZAIDI  HAPA 

No comments: