Staa mrembo kutoka Bunge Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amempongeza muigizaji mwenzako wa kitambo, Monalisa kwa kusema kuwa amekuwa akifundishwa kuwa na subira kwenye maisha kupita muigizaji huyo.
Akizungumza wakati wa tuzo za African Women Film Festival zilizofanyika hivi karibuni, Lulu alisema Monalisa ameanza kazi za Sanaa muda mrefu , lakini amekuja na wazo hilo la kutoa tuzo sasa hivi.
“Wasanii huwa tunakuwa na mambo mengi ya kufanya pale tunapopata maarufu, lakini Monalisa hilo kwake halikuwa sababu, kwani amekaa kimya kwa muda wote mpaka sasa alipoamua kuja na tuzo hizi ambazo naamini huko mbele zitakuwa kubwa,” alisema.
“Sisi kama watu ambao tunakutizama tangu, mabinti wadogo tumekuwa tukikuona kwamba kumbe kila kitu kinawezekana, Halafu pia kikubwa umetupa somo la kusubiri, katika muda sahihi. You have been Monalisa for such a long time, lakini umefanya mambo yako taratibu, yani hajakurupuka ili uonekane monalisa leo amefanya tuzo, but you took your time , umeenda taratibu mpaka leo umeweza kufanya hivi.”-Lulu alieleza.
Mbali ya kualikwa kwa ajili ya kutoa tuzo, pia alikuwa kati ya wasanii waliokuwa wakiwania kipengele cha msanii bora wa filamu ambacho muigizaji Riyama Ally aliibuka kidedea.
Wengine walioshindanishwa katika kengele hicho ni Neema Ndepanya, Lamata Leah na Godliver Gordian.
0 Comments