LULU AFUNGUKIA NDOA YAKE NA MAJAY - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 17, 2019

LULU AFUNGUKIA NDOA YAKE NA MAJAY

Staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amezungumzia kuhusu ndoa yake talajiwa na CEO wa EFM, Majay.“Mimi na mwenza wangu Majey bado hatujaoana. Sisi tabia zetu zinaendana ni watu wa kawaida hivyo tutafunga ndoa kawaida yaani ndugu upande wa kiume na upande wa kike pamoja na marafiki zetu baadhi. Baby wangu sio tajiri bali ni mtu ambaye ameanzia chini kimaisha mpaka kufika alipofika na am proud kwa hilo”-Lulu amesema.

Lulu amefunguka hayo leo kwenye  kipindi cha XXL cha Clouds FM ambapo pia alizungumzia kuzipuuza stori za yeye kusemekana kumteka kishirikina mpenzi wake huyo.

“Story ambazo zilikuwa zinasambaa mitandaoni kuwa nimemuwekea ‘Limbwata’ mpenzi wangu, niliziona kwenye mitandao ya kijamii kama wengine walivyoziona na kiukweli hazikuniumiza kabisa maana mwanzoni zilikuwa zinanipa shida sababu nilikuwa nazifatilia lakini kwa sasa sizipi nafasi ya kuzifatilia maana kitu unavyokipa nafasi ndivyo kitakavyo kuumiza”.-Lulu alieleza.

Lulu ni miongoni wa mastaa wenye majina makubwa sana hapa chini kwenye upande wa uingizaji kwani sanaa hiyo ameianza tangu akiwa na umri mdogo.
Loading...

No comments: