LULU:KIFUNGO KIMENIFUNDISHA KUWA MAKINI NA WANAUME - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, April 18, 2019

LULU:KIFUNGO KIMENIFUNDISHA KUWA MAKINI NA WANAUME

Staa wa Bongo Movie, Elizabeth Michael 'Lulu', amesema moja ya sababu za wanawake kujikuta magerezani ni mikasa inayohusiana na wanaume.Lulu ameyasema hayo janaJumatano Aprili 17,2019 akihojiwa na kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds FM.
Msanii huyo aliyewahi kutamba na filamu za Family Disaster, Foolish Age na A Woman of Principle, alihukumiwa kwenda jela miaka miwili Novemba 13, 2017 baada ya kupatikana na hatia kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba na kuachiwa huru Novemba 12, 2018 kwa msamaha wa Rais.
Lulu amesema kwa muda wote aliokuwa akitumikia kifungo chake gerezani kwa kila aliyejaribu kumuuliza kisa cha kufikishwa huko, wengi walihusisha wanaume.
“Mtu amekutwa na hatia kutokana na kosa la kuiba na ukichimba zaidi anasema mwanaume ndiye alimsababisha kuiba ili wawe na maisha mazuri, au wakati mwingine alimwekea dhamana mpenzi wake mwisho wa siku akatoroka,” amesema Lulu.
Kutokana na matatizo hayo, amesema kuna kila sababu ya kuangalia namna ya kutibu mizizi hiyo kwa kuwa wanawake wamekuwa wakiteseka kwa ajili ya wanaume.
Loading...

No comments: