MAKONDA AFICHUA ALICHOTENDEWA NA DKT. MENGI AKIWA CHUONI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefichua kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi alimchagia ada wakati akiwa chuo na kufika hadi kwende chumba chake alipokuwa chuoni,wakati hakuwa na ndoto ya kuja kuwa Mkuu wa Wilaya, au kiongozi vyuo Vikuu.

Dr.Reginald Mengi na Paul Makonda

Makondo ameyasema hayo leo katika hafla ya utoaji wa vyeti vya sifa kwa askari mbalimbali waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2018, iliyofanyika uwanja wa kituo cha polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kenye hafla hiyo Reginald Mengi amewapa wajane 10 wa askari wa jeshi la polisi Sh2 milioni kila mmoja kama kifuta machozi kutokana na kuwapoteza waume zao wakiwa kazini

Katika hafla hiyo Polisi waliofanya vizuri walipewa zawadi mbalimbali ikiwamo pikipiki, saruji mifuko 10, mabati na fedha kama kifuta machozi kwa wajane ambao waume zao wamefariki wakiwa kazini.Post a Comment

0 Comments