MAMA WEMA AFUNGUKIA ISHU YA WEMA NA DIANA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 3, 2019

MAMA WEMA AFUNGUKIA ISHU YA WEMA NA DIANA

Kufuatia minong’ono kuibuka mtandaoni yakitilia mashaka mahusiano ya karibu baina ya waigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu na Diana Kimary, Mama Mzazi wa Muigizaji Wema Sepetu, ametoa yake ya moyoni hayo nakusema akiwa kama mzazi wa muigizaji huyo, amechoka na vitendo vya muigizaji Diana kwa kuwa anamrudisha nyuma mtoto wake kiasi cha kushindwa kufanya maendeleo.


Wema Sepetu na Diana Kimary

Kwa mujibu wa sauti iliyosambaa mtandaoni ambayo inadaiwa kuwa ni ya mama Wema, akiwa kama mzazi ameongea kwa uchungu kuchukizwa na ukaribu wa Wema na Diana kwani hauna faida wala maendeleo kwa mtoto wake na kuwataka wapenzi wakweli wa mtoto wake waendelee kumsema ile abadilike.

“Nianchokata Wema ajitambue, Wema abadilike, Wema ajue anafanya nini, naiumua sana kama mama mzazi, naumia sana nianpoona Wema hataki kusikia” –Sauti inayodaiwa kuwa ya mama wema inasikika.

Mama wema amesema atakula sahani moja na Diana kuhakikisha anamtenganisha na Wema kwani anaamini nazi haiwezi kushindana na jiwe.

"Huyo Diana nimeshampiga nitaendelea kumpiga mpaka nihakikishe namvunja mguu",

imesema sauti hiyo inayodaiwa kuwa ni ya mama Wema.

Pamoja na hayo mama wa muigizaji huyo amewataka mashabiki na watu wa karibu wa Wema wamuambie ukweli kuhusu matendo anayoyafanya hata kama atawachukia.

“Naombeni mnisaidie hata awapige block wote lakini mwambieni ukweli na ukweli ndiyo unamfana mtu ajitambue”-Ikiendelea

Urafiki wa karibu baina ya Wema Sepetu na Diana umekuwa wakaribu mno kufikia hatua hadi Diana kujichora tatoo ya Wema Sepetu mwilini inavyoonekana hapo chini.

Loading...

No comments: