LEMA AJIBU KUHUSU DENI ANALODAIWA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, April 5, 2019

LEMA AJIBU KUHUSU DENI ANALODAIWA

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema  amedai kuwa kudaiwa sio kosa na ataendela kukopa na hajawahi kushindwa kulipa. Hii ni baada ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza  bungeni deni la zaidi ya milioni 400 ambalo Godbless Lema anadaiwa na kwamba ndio chanzo cha msongo wa mawazo kwa mbunge huyo wa Arusha Mjini (Chadema).

Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema

Lema alisema hayo jana muda mfupi baada ya Bunge kupitisha azimio la kumsimamisha mikutano mitatu kuanzia mkutano huu.

“Spika kama alifikiri ananidhalilisha hajafanikiwa kwani mimi kudaiwa sio dhambi na nitaendelea kukopa.” alisema Lema.

“Hata jengo la Bunge likiwa linakopeshwa nitalikopa, kwani sijawahi kushindwa kulipa, wabunge wengi wana mikopo hata Spika mwenyewe anaweza kuwa anadaiwa lakini kama hadaiwi basi ni yeye,” alisema aliongeza.
Kuhusu kauli ya Ndugai kuwa ana msongo wa mawazo, mbunge huyo alisema: “Hili nawaachia wananchi wapime kati yangu na Spika Ndugai nani mwenye msongo wa mawazo.”


Mbunge huyo ameadhibiwa kutokana na kuunga mkono kauli iliyotolewa na mbunge mwenzake wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) kuwa Bunge ni dhaifu ambaye naye amesimamishwa vikao viwili.


LEMA ATOA NENO BAADA YA KUSIMAMISHWA
Loading...

No comments: