MITINDO HAINA UHUSIANO NA USHOGA- MUSTAFA HASSANALI

MUSTAFA Hassanali ni jina kubwa kwenye tasnia la ubunifu na mitindo ya mavazi, huku akiwa ni miongoni mwa watu waliofanikisha kuikuza na kuendeleza sanaa hiyo kwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Mustafa Hassanali
Katika safu hii, Hassanali ameweza kuzungumzia mambo mbalimbali na namna alivyoweza kupenya kutoka Tanzania hadi kufikia masoko makubwa ya kimataifa, ikiwemo Afrika Kusini na Italia.
KUPATA TUZO
‘’Ninachojivunia katika maisha yangu ya fasheni ni kuweza kutwaa tuzo ambayo nilipewa nje ya nchi, tuzo ya kuwa mbunifu bora wa kiume Afrika Mashariki.
SWAHILI FASHION WEEK
‘’Swahili Fashion Week imekuwa mkombozi wa wabunifu wa Tanzania kuweza kutambulika zaidi na kuweza kupata wabunifu wenye viwango, Ally Remtullah, Martin Kadinda, Asia Idarous Khamsi na wengine wengi wameweza kujitambulisha Afrika Mashariki kupitia Swahili Fashion Week.
MITANDAO YA KIJAMII
‘’Mitandao ya kijamii imesaidia kukuza kazi zetu za fasheni, kwani watu wamekuwa wakijionea mitindo mbalimbali na kuweza kuwatafuta wanamitindo na kutaka kushonewa nguo ambazo wanaona kwenye mitandao ya kijamii.
NAMKUBALI DIAMOND
‘’Kitu ambacho kinanifanya nimpende zaidi Diamond ni kutokana na kuweza kutumia nafasi yake ya kukuza sekta ya mavazi, kwani Diamond ni msanii pekee ambaye anaweza kuvaa kwa kutumia wanamitindo wa Tanzania.
UHUSIANO WA MITINDO NA USHOGA
“Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha mitindo ya mavazi na tabia au vitendo vya kishoga. Niseme jambo moja kwamba hii ni kazi yenye heshima yake. Wanaofanya ushoga ni tabia zao wenyewe kama wapo, lakini kwenye sanaa nimekaa muda mrefu lakini sijaweza kuona mambo hayo yanayosemwa.
“Vilevile jamii inafaa kutambua kwamba hii ni kazi ambayo ina kipato kikubwa na kuacha imani potofu kwamba sanaa hii ina mambo ya kishoga ndani yake, jambo ambalo si kweli,’’ anasema Hassanali.

Chanzo:Dimba

Post a Comment

0 Comments