MSALABA NA MADHABAHU YA KANISA VYANUSURIKA KUUNGUA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 16, 2019

MSALABA NA MADHABAHU YA KANISA VYANUSURIKA KUUNGUA

Moto mkubwa ulizuka katika kanisa hilo kongwe la Notre-Dame mjini Paris Ufaransa mwendo wa saa kumi na mbili na nusu kwa saa ya huko - jengo ambalo ni moja ya makanisa maarufu na linalotembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka pande mbali mbali duniani kila mwaka.Sehemu kubwa ya paa la majengo ya kanisa hilo yameteketezwa na moto huku mwingine ukifanikiwa kuzimwa katika minara miwili ya kengele.

Picha za mwanzo za ndani ya kanisa kongwe la Notre-Dame baada ya moto zimepatikana na kuonesha kuna baadhi ya maeneo ya kanisa hilo hayajaungua.Baadhi ya maeneo muhimu ambayo hayajaunguzwa katika mkasa huo ni madhabahu na msalaba, mimbari pamoja na baadhi ya mabenchi.

Maafisa wa zima moto walifanikiwa kuliokoa jengo hilo la historia lenye miaka 850 lakini paa na mnara wa jengo hilo yameanguka.
Moto huo ulidhibitiwa saa tisa baada ya kuanza, na kuzimwa kabisa baada ya saa 16.

Rais wa Ufaransa ameahidi usaidizi wa kimataifa katika kulijenga upya kanisa kongwe.

Tayari mamilioni ya Dola yameahidiwa na watu mbali mbali duniani ili kusaidia ukarabati wa kanisa hilo.

Chanzo chake hakijajulikana lakini maafisa wanasema huenda ukahusishwa na ukarabati mkubwa unaoendelea.
Loading...

No comments: