Mshtakiwa wa Kwanza wa Mauaji ya Rapper Nipsey Hussle Atajwa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 3, 2019

Mshtakiwa wa Kwanza wa Mauaji ya Rapper Nipsey Hussle Atajwa


Mshtakiwa wa Kwanza wa Mauaji ya Rapper Nipsey Hussle Atajwa

Mshtakiwa wa Kwanza wa Mauaji ya Rapper Nipsey Hussle Atajwa
Leo April 2,2019 taarifa zimetolewa na polisi wa Los Angeles nchini Marekani na kudai kuwa wamembaini mhusika anayetuhumiwa kumuua Rapper Nipsey Hussle nje ya duka lake la nguo ‘The Marathon Clothing” Jumapili ya March 31,2019.

Mtuhumiwa huyo ambaye ametambulika kwa jina la Eric Holder’29 na kwa sasa inaripotiwa kuwa anasakwa na idara ya polisi ya Los Angeles kwa mauaji hayo pamoja na wengine wawili waliopoteza uhai kwenye shambulio hilo.

Siku ya Jumatatu April 1,2019 maelfu ya mashabiki walijitokeza nje ya duka la Rapper huyo na kuomboleza huku wengine wakiimba nyimbo zake tofautitofauti na baadae sauti za risasi kusikika na watu kuanza kukimbia lakini baadae sauti hizo zilihusishwa na milio ya chupa pamoja na baruti na kuripotiwa kuwa sio risasi. 


Loading...

No comments: