MSIMU WA TATU WA “SMIRNOFF ICE BLACK DJ SEARCH” WAMALIZIKA, WASHINDI WAJIZOLEA ZAWADI

Mmoja wa majaji wa Shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ Immanuel John maarufu kama ‘DJ Summer’ akizungumza wakati wa fainali za shindano hilo zilizofanyika Jumamosi, April 13 , 2019 jijini hapa.
Hatimaye msimu wa tatu wa wa shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ kwa mwaka 2019 umemalizika huku DJ KG akiibuka mshindi kwa kuwapiku maDj sita walioshiriki kwenye fainali hizo.

DJ KG kutoka Mkoa Dar es Salaam alitangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa shindano hilo ambapo jumla ya maDJ sita walishiriki na kudhaminiwa na kinywaji cha Smirnoff Ice Black kinachozalishwa na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).

Akizungumza wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbu wa Life Park Mwenge, Meneja wa bidhaa wa SBL Ester Raphael alisema lengo ni kuibua vipaji vipya kweye tasnia ya muziki kupitia fani ya uburudishaji ‘DJ’ sanjari na kutoa hamasa kwa wateja wa bidhaa zao.

Mtangazaji maarufu nchini, Hamisi Mandi maarufu kama B-Dozen akimpongeza mshindi wa shindano la ‘Sminorff Ice Black Dj Search’ ‘DJ KG’ baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza wa fainali hizo kwa mwaka 2019.
“Tunaamini kwa kupitia shindano hili, SBL itatoa msisimko kwa wateja wake na muziki mzuri na nafasi ya kipekee kuonyesha uwezo wa MaDj wanaochipukia,” alisema

Shindano hilo limefanyika katika mikoa mitano ikiwamo Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Mwanza na Arusha ambapo waliweza kuwapata maDj sita waliotinga hatua ya fainali.

Alitaja zawadi zinazotolewa kwa washindi ikiwamo vifaa vya Dj “Dj Kit,Laptop pamoja na Conrollers kwa washindi watatu.

“Ushindani wa msimu huu ni mkubwa sana na tumeona Madj wakipamana kwa hali na mali na hamasa imekuwa kubwa sana kwao na kwa wateja wa kinywaji chetu cha Smirnoff Ice Black,” alisema 

Mmoja wa washiriki wa shindano la ‘Smirnoff Ice Black Dj Search’ akionyesha ujuzi wake wakati wa fainali zilizofanyika Jumamosi jijini hapa.

Katika fainali hizo, DJ KG kutoka Mkoa wa Dar es Salaam aliibuka mshindi wa kwanza na kuibuka na DJ kits pamoja na Laptop (Mac).

Mmoja wa Majaji, Immanuel John ‘DJ Summer Tz’ alisema walizingatia zaidi ujuzi wa DJ pamoja na muitiko kutoka kwa watu wanaowasikiliza.


Post a Comment

0 Comments