MWANAUME AKIJA KWANGU LAZIMA AJIPANGE- CHEMICAL

Msanii wa Kike anayechana na kuimba kutoka kiwanda cha Bongo Fleva, Claudia Lubalo 'Chemical' anayetamba na ngoma ya ‘Nitajioa’, amefunguka kuwa wanaume wamekuwa wakiogopa kumsumbua kimapenzi kutokana na staili yake ya kujiweka kigumu.

Claudia Lubalo 'Chemical'

Chemical amesema kuwa wasanii hasa wa kike hupitia mambo mengi ikiwamo kulazimishwa kutakiwa kimapenzi, lakini kwake ishu hizo hazipo.

“Yaani huyo mwanaume akija kwangu lazima ajipange kwelikweli na awe na malengo, sio eti mtu anakuja kujaribu tu. Si unaona mwenyewe mikato yangu sasa lazima nimbane mtu,” alisema.

Alisema ni kutokana na hilo ndio sababu ya kuachia ngoma ya ‘Nitajioa’ ambayo, pamoja na mambo mengine inazungumzia wanawake wanaoishi maisha ya kigumu kama staili yake.

Hata hivyo, alisema kuwa licha ya jamii kuwachukulia tofauti kuwa hawawezi kuwa wake bora wa kuishi na wanaume, ukweli wanaweza kuolewa na wakawa wazuri ndani ya familia zao.

Kuhusu mipango ya kuwa na familia, Chemical alisema bado sana.

Post a Comment

0 Comments