Mwinjaku Aishukia WCB Kumruhusu Mbosso Kupost Nyumba na Kudai ni yake Wakati sio Kweli - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 3, 2019

Mwinjaku Aishukia WCB Kumruhusu Mbosso Kupost Nyumba na Kudai ni yake Wakati sio Kweli


Mwinjaku leo tena aja na jipya baada ya Msanii Mbosso kupost picha ya Nyumba ambayo anadai ameinunua baaada ya Mafanikio akishirikiana na Managnment yake

Mwijaku amejirekodi akiponda uongozi wa WCB na kudai iweje wamruhusu mbosso aseme nyumba ni yake amenunua wakati si kweli

Nanukuu "Imefika muda inabidi tuwe wakweli tuweze kuwasaidia watoto, wasaniii na watu wenye vipaji Maalum, Hakuna kitu kinachoumiza kama Unamtumia Msanii kudanganya jamiii kuwa yeye amefanikiwa kutokana na kazi yake anayoifanya wakati si kweli, Kitendo cha WCB kwenda kumuhadaaa Mbosso akae na kuiambia jamiii kuwa anamiliki nyumba wakati si kweli ni kitendo ambacho mnamwaribia mtoto, akitokea mtu mwingine anataka kumzamini ataogopa coz anajua kashafanikiwa" Mwinjaku

Mbosso ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram na kupost nyumba anayodai ni yake

"Reposted from #mbosso_  -  Mwenyezi Mungu ni Mkubwa sana na anasiri kubwa sana katika kila ya mja wake (..Asante Mola wangu..)..., huenda hiki kikawa kidogo sana kwa wengine ila kwangu Mimi nikikubwa sana , tena sana kwa sababu sikuwa na uwezo nacho  awali, ila tu Mapenzi yenu na Sapot yenu kwangu mmenifanya leo hii na Mimi niwe na kwangu .., "Eti Mbosso na Mimi leo nina kwangu 😭.." , "Acha niseme asanteni sana kwa upendo wenu, asanteni kwa Kuokoa kipaji changu na kuamua kunisapot tangu siku ya kwanza hadi kufiki leo hii .." Hiki ni kidogo mulichoweza kunifanya nimiliki  leo hii kijana wenu.. "Mungu awabariki sana na awafungulie milango yenu ya rizki kwa upana zaidi " ili mupate nguvu ya kuendelea kunisapot Kijana wenu " inshaalla"🙏" 
Loading...

No comments: