MIMI SIJAFA,NIPO MZIMA- MZEE WA UPAKO

Kupitia video fupi iliyosambaa mtandaoni, Mchungaji wa kanisa la Maombezi la GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’, amejibu taarifa za kuzushiwa kifo, na kusema kuwa yeye hajafa.

Mchungaji wa kanisa la Maombezi la GRC la jijini Dar es salaam, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’
Akionekana mzima wa mwenye afya Mzee wa Upako alisema haya;

“Eti nini!?, nimekufa!?. Mimi sijafa, wala siumwi hata mafua, niko mzima, watu wangu wote muwe na amani, eti nini!!? nimekufaa!!. Nitabaki kuwa juu, nitabaki kileleni.”Mchungaji Lusekelo alimalizia taarifa hiyo huku akipiga kionjo cha Piere Mzee wa Liquid, huku akifurahi. 

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikisema kuwa Mchungaji huyo hali yake ni mbaya kiafya, huku zingine zikisema kuwa ameshafariki dunia.

Post a Comment

0 Comments