Ishu ya Ruge Yaibuka, Uzinduzi wa Albamu ya Nandy Kenya - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 29, 2019

Ishu ya Ruge Yaibuka, Uzinduzi wa Albamu ya Nandy Kenya

Staa mrembo wa Bongo Fleva, Nandy amezindua albamu yake ya kwanza the ‘African Princess’ kwa staili ya kipekee jana Jumapili kwenye ukumbi wa kifahari wa Golden Bistro, Nairobi.


Nandy aliyeongozana na msanii Willy paul anayedaiwa kuwa wapenzi, alitumbuiza nyimbo zote 13 ambazo zote ni kazi solo, tisa zikiwa mpya kabisa.

Nandy alisema Kenya nina mashabiki wengi hivyo baada ya kufanya uzinduzi Tanzania Novemba mwaka uliopita niliona ni freshi kama nikaja huku na kufanya hivyo pia.

Uzinduzi huo ulifanyika siku iliyofanyika ibada ya wafu ya kumkumbuka mdau wa mkubwa wa burudani nchini Tanzania, Ruge Mutahaba ambaye chini ya lebo yake ya Tanzania House of Talent ndiko alitokea Nandy.

Nandy alikuwa na ukaribu na Ruge na kudaiwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi naye hivyo kukosa kuwepo kwenye siku hiyo maalumu ya kumuenzi, kuliibua maswali.

Akizungumza kwa nini asingeisogeza mbele uzunduzi wa albamu yake ili kupata muda wa kumuenzi Ruge, Nandy alijitete kwa kusema “hili lilikuwa limeshapangwa tayari hata kabla ya Ruge kufariki. Hivyo kuahirisha ingevuruga mambo mengi ya kibiashara kwa upande wangu na wale nilioshirikiana nao. Sikuwa na jinsi.”
Loading...

No comments: