"NAS NI RAPA NINAYEMKUBALI KWA MUDA WOTE" ASEMA JENNIFER LOPEZ


Utakubaliana na mimi kuwa kila mtu anayependa mziki huwa na orodha ya nyimbo kali au wasanii wakali japo watano anaowakubali kwa kufanya kazi zao vyema na wanavyomgusa kwa ubunifu, mashairi na hata performance jukwaani. 

Sasa alipoulizwa "yupi ni msanii wako mkali wa Hip Hop duniani kwa muda wote?" bila kupepesa macho bibie Jennifer Lopez alimtaja Nas. 

Supastaa huyo aliyasema hayo akiwa kwenye show ya mahojiano na mtangazaji Elliot Wilson wa kipindi cha CRWN. 

JLo alieleza kwa undani zaidi kwa kusema kuwa Nas kwake ni mkali wa rap kwa muda wote, na ni namba moja, na akamalizia kwa kusema kuwa hajawahi kusikia msanii yeyote anaye-rap kama Nas

"Nas is one of my favourite rappers of all time, He might be number one. I don't think I've heard anybody who raps, who hits me in the same way. He sounds like guys I grew up with, but he's so intelligent." alisema JLo.

Baada ya maongezi hayo JLO aliombwa ataje top 5 ya wasanii anaowakubali kwa muda wote ambapo aliwaongeza Pun, Fat Joe, Biggie na Lil Wayne. 

Post a Comment

0 Comments