NJOONI KWA MUNGU MNG’AE - MUNA LOVE

Mwigizaji na mwanadada aliyepata umaarufu Instgram,Rose Alphonce maarufu kama 'Muna Love' amewashangaa baadhi ya watu wanaojadili picha zake anazopost kwenye ukurasa wake wa Instagram, na kuwauliza, “Kwani na wao wanataka kung’aa kama mimi?”

Muna Love

Hivi karibuni akiongea na mtandao wa clouds FM, Muna Love alisema;

“Watu walishazoea siku zote mtu akiwa ameokoka anakuwa hapendezi anakuwa tofauti wakati kwa Mungu kuna kila ambacho unakihitaji, kuna kila kitu ambacho unamwomba wewe atakupatia kwa sababu umemwambini na kumpa maisha yako, nimemwamini na kumpa maisha yangu Mungu anaangalia moyo wangu haangalii kuwa nimevaa hivi.’’

‘’Yeye ndiye anayenibariki na kuniongoza kwahiyo hata kupendeza kwangu kunatokana na kung’arishwa na Mungu, angekuwa haning’arisha nisingependeza, kwani wangapi wanapendeza na kuvaa nina kitu gani cha ajabu mpaka kikamstua mtu, hiyo picha ni ya kawaida sana lakini kwa sababu Mungu ndio maana wanaiona ya tofauti’’  Muna Love aliongeza.

Aidha Muna Love amesema maisha yake ya nyuma na ya sasa ni tofauti kwa sasa ana furaha, amani na anamtukuza Mungu kwa kila kitu, na amewaambia watu wanamjadili waende kwa Mungu na waone kama anaweza kuwazuia na wao kung’aa.
Post a Comment

0 Comments