OFISI YA BUNGE IMEKANUSHA SPIKA JOB NDUGAI KUMTAKA CAG, PROF. MUSSA ASSAD AJIUZULU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 17, 2019

OFISI YA BUNGE IMEKANUSHA SPIKA JOB NDUGAI KUMTAKA CAG, PROF. MUSSA ASSAD AJIUZULU

Ofisi ya Bunge imekanusha kuwa Spika Job Ndugai hajaandika barua inayotoa wito kwa CAG, Prof. Mussa Assad kujiuzulu ama kujieleza kwa mwajiri wake kwanini asiadhibiwe. 

 
Ofisi hiyo imewatahadharisha wananchi dhidi ya uzushi huo ikisema, ufafanuzi wa azimio dhidi ya CAG ulishatolewa.

Taarifa maalum kutoka kitengo cha mawasiliano ya Bunge, imesema kuwa barua hiyo hawaitambui na si ujumbe wa Spika Job Ndugai kwenda kwa CAG, Prof. Assad.

Taarifa hiyo imesema kuwa, "kumekuwepo kwa taarifa nyingi za uzushi kupitia mitandao ya kijamii, tangu Spika Job Ndugai azungumze na waandishi wa habari, moja wapo ni barua ya yenye kichwa cha habari "wito wa ama kujiuzulu au kujieleza kwanini usiadhibiwe na mwajiri wako".

Tunatahadharisha umma barua hiyo ni ya uzushi hivyo ipuuzwe, ofisi ya Spika na ofisi ya Bunge haihusiki kwa namna yeyote na barua hiyo".


Isome hapa zaidi: 
Loading...

No comments: