RAIS MAGUFULI AMSHAURI WAZIRI KUVUTA BANGI YA NJOMBE

Leo  aprili 11, 2019 akiwa ziarani Makambako Mkoani  Njombe, Rais Dr John Magufuli amemshauri waziri wa Maji kuwa mkali anapoenda kutana na makandarasi wa miradi ya Maji.
Rais Dr John Magufuli
Akiongelea kutolidhishwa na mwendendo wa miradi ya maji, Rais Magufuli  alisema haya kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Makame Mbarawa;

"Nimekupeleka pale ukafanye mabadiliko, ukalisimamie hilo, kwa sababu nina matatizo sana na baadhi ya miradi ya maji, na ndio maana nimekuwa nikifanya mabadiliko kwenye miradi ya maji, kwa sababu haileti impact.  Zinazungumzwa fedha zimeenda kwenye miradi lakini hazikuenda, kuna wakati nilienda kanda ya ziwa, mradi umetumika milioni 400, zilikuwa milioni 800  lakini maji hayapo, sasa nikuombe Waziri na watendaji mkawe wakali kweli kweli, kama unaweza ukavute bangi ya Njombe ili uwe mkali kaivute, kaivute kisiri siri wasikuone ukiivuta, ili ukienda kwenye mradi hawa mainjia wa maji wakafanye kazi”, amesema Rais Magufuli.

KatIka hatua nyingine Rais Maguful ameagiza wahandisi wote wa maji kwenye halmashauri za wilaya kuhamia Wizara ya Maji, ataka wahandisi wasiofanya vizuri kufutwa kazi.

Post a Comment

0 Comments