RAIS MAGUFULI AMWAGA AJIRA KWA VIJANA WA JKT

Rais, John Magufuli ametoa ajira kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) zaidi ya 2,000 walioshiriki ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali.


Vijana hao ni walioshiriki kwenye ujenzi wa nyumba za Serikali, ukuta wa Ikulu ya Chamwino Dodoma, nyumba za magereza pamoja na wanaofanya kazi kwenye kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mji wa kiserikali wa Ihumwa Dodoma leo, Rais Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na kazi kubwa iliyofanywa na vijana hao kwa muda mfupi na gharama nafuu na moyo wa kujitoa kwa ajili ya taifa lao.
Ameelekeza vijana hao waajiriwe katika maeneo mbalimbali ikiwamo jeshini, usalama wa taifa, Takukuru, uhamiaji na taasisi nyingine za Serikali.
Sambamba na hilo, Rais Magufuli amempandisha cheo kiongozi aliyekuwa akisimamia kazi hizo za ujenzi, Kanali Charles Mbuge kuwa Brigedia Jenerali.
Mara baada ya kumtangaza alimuita mbele Brigedia Mbuge kwenda kukaa kwenye jukwaa kuu sehemu inayotengwa kwa ajili ya viongozi wakuu.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa upo umuhimu wa jeshi kuanzisha kikosi cha ujenzi kwani linafanyakazi kwa ufanisi mkubwa, huku akimuelekeza Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo kuwapa motisha wanajeshi walioshiriki kwenye kazi hizo.
Awali, Jenerali Mabeyo alimwomba Rais Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kusema neno moja tu ambalo litawapa faraja vijana hao

Post a Comment

0 Comments