RAIS MAGUFULI AZUNGUMZIA UNUNUZI WA KOROSHO, KANGOMBA WAPONA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 2, 2019

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZIA UNUNUZI WA KOROSHO, KANGOMBA WAPONA

Leo  Aprili 2, 2019, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  amewasili mkoani mkoni Mtwara kwa ziara ya kikazi.Ameweka jiwe la msingi la upanuzi wa Uwanja wa ndege na kuzungumza na Wananchi.

Hapa akizungumza na wananchi wa mkoa huo.

Nimekuja kutembelea mkoa wa Mtwara; nataka kuwaambia watu wa Mkoa huu na watanzania wote nawapenda sana. Nadhani nimekuja wakati muafaka, na napenda kuwashukuru wote pamoja na viongozi. Mara ya mwisho nilikuja mwezi Machi 2017

Serikali inapanua uwanja wa Ndege wa Mtwara kwasababu ya uchakavu wa miundombinu. Ulijengwa miaka ya 1952 hadi 1953. Sasa uwanja hauwezi ukajengwa kwa mahitaji ya miaka ya 1952 halafu ukatumia miaka hii, tunaujenga uwe wa kisasa

Katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara, tunaongeza urefu wa njia ya kurukia kutoka mita 2,258 hadi mita 2,800 na upana kutoka mita 30 hadi mita 45. Tutaweka taa ili ndege ziweze kutua hapa mchana au usiku uwanja ukikamilika

Upanuzi wa uwanja wa Ndege Mtwara utagharimu Tsh. Bilioni 50.366 ikiwa zote ni pesa za kodi za wananchi. Na muda aliopewa mkandarasi wa kufanya "mobilization" ambapo alitakiwa awe ameshamaliza, lakini bado kwani anadai fedha

Nikamuuliza Waziri wa Uchukuzi, “Umeshamuuliza Waziri mwenzako wa Fedha?” akasema bado. Hili nalo ni tatizo kwa Mawaziri kutowasiliana. Kwasababu wangekuwa wanawasiliana hizo fedha za mobilization zingekuwa zimetolewa

Sasa natoa siku tano (5) kwa Mawaziri hawa fedha, hizo za mobiliization ziwe zimefika kwa mkandarasi. Na huyu mkandarasi namuambia kuwa nimeona kazi alizofanya Mwanza sio nzuri, na nashangaa amepewaje hii kazi

Sasa nataka kumuambia huyu Mkandarasi atakapozitapa hizi fedha 10% ni Bilioni 4.5 na 15% ni Bilioni 7.5, ninyi mpeni hizo asilimia 15. Ndani ya siku 5 mpeni hizo pesa! Sasa asifanye kazi, haki ta Mungu atakoma, afanye kazi usiku na mchana

Huwezi kuja wakati wa mobilization unakuta malori mawili utafikiri ni ya kubeba korosho. Na yale yameegeshwa tu! Hata hili greda nimeliangalia matairi ya mbele yameisha. Tufike sehemu watanzania tuseme ukweli

Miradi mingine muhimu inayotekelezwa Mtwara mbali na mradi huu, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara pale Mikindani. Gharama za mradi huu ni Tsh. bilioni 23.843 ambapo mpaka sasa Tsh. Bilioni 5.68 zimetumika

Serikali imetoa Tsh. Bilioni 10.3 kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya Afya Mtwara. Tsh. Bilioni 5.8 kwa ajili ya kukarabati vituo vya afya 13 na Tsh. Biloni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali za wilaya hapa Mtwara, Nanyambana Masasi

Suala la Serikali kuamua kununua korosho kila mmoja anajua, ni pale mwaka jana bodi ya korosho na wadau walipoamua inunuliwe kwa ya Tsh. 1,500-2,100. Lengo lilikuwa kuwanyonya wakulima, mimi mtoto wa mkulima nafahamu shida za kilimo

Nikasema hawa wakulima wanaodhulumiwa walinichagua mimi na walitaka nikawatetee, nikaangalia Serikalini nikaona fedha zipo. Nikasema tukanunue hizi korosho kwa bei kubwa, na nikasema korosho zitanunuliwa kwa Tsh. 3,300 kwa kilo

Tulivyopiga hesabu tukaona korosho hizo zitazidi kidogo tani laki 2. Tulivyofanya uhakiki ktk mikoa yote kuna korosho 224,964. Tani 2,139 zilikuwa zimekusanywa kabla Serikali haijaingilia. Tani zilizotakiwa kulipwa na Serikali ni 222,000

Tulianza na wananchi ambao walikuwa na kilo chini ya 1,500 kwa sababu lazima kuwe na utaratibu popote pale. Walikuwa 390,765 na walikuwa na tani zaidi ya 160,669.3 zilizokuwa na gharama ya Sh. Bilioni 521.8

Wakulima 373,149 wamelipwa walikuwa na tani 156,855.2. Wakulima 17616 hawajalipwa wenye kilo 1500 - Hawajalipwa kwa sababu nyingi tu ikiwemo waliwekewa fedha kwenye benki ambapo akaunti ina jina ni tofauti na lake

Wapo waliotoa maelezo na wakabadilisha, wakafungua akaunti na kadhalika, karibu asilimi 98 hadi 99 wamalipwa na orodha yao ninayo. Kila aliyelipwa kwa wakulima hao wenye kilo chini ya 1500 orodha yao ninayo, kila Wilaya na kila Mkoa

Katika hao waliolipwa wapo waliokuwa na madeni, sasa anapokuja mwenye deni anasema 'sijalipwaaa aisee koroshooo' - Wapo wanaume unakuta na wake 2 hadi 3, anapeleka fedha nyumba ndogo. Nyumba kubwa ikiuliza anasema ‘korosho'

Wote waliolipwa orodha ipo na Mkuu wa Mkoa sasa nenda kawaumbue Mtu akizungumza hajalipwa na kwenye orodha ya malipo yupo, kamata na weka ndani

Wapo wale waliokuwa na kilo 1500 na zaidi ambapo uchambuzi umekamilia na walikuwa 18,103, hao hawajalipwa. Sasa uchambuzi wake umekamilika, tusingelipa bila uchambuzi. Majina 780 yamepatikana hawana mashamba wala mkorosho

Nataka kuwaambia ndugu zangu, hawa wenye majina 18,000 Waziri wa kilimo yupo hapa na wa Biashara yupo hapa. Nimetoa maagizo nikiwa Dar ziletwe Bilioni 50, kuanzia kesho au kesho kutwa hawa nao waanze kulipwa, zikiisha tunaleta nyingine

Wale waliokiri ni makangomba na walinunua korosho na zimechukuliwa na Serikali na walifanya kosa kwa kununua mahali ili wapate faida. Nasema hao nao tuwaangalie, tuwalipe. Najua waliofanya hivyo ni wengi mpaka Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa

Lakini nataka wakiri kuwa “Mimi nilinunua korosho kwa mtu fulani, sina shamba” na akisema “Naomba mnilipe tu kwa kuwa nilikuwa nafanya bishara”. Nafikiri walikuwa ni hawa 780 lakini siku nyingine kwenye msimu mwingine wasirudie

Najua ‘Kangomba’ imekuwa habari ya kila mtu lakini nataka wakiri, waandike kuwa nina kangomba kiasi fulani. Wote nimewasamehe. Wasirudie kuwaumiza wananchi hawa wadogo na sisi viongozi tusiwaumize wananchi

Hatuwezi kulipa holela na ndio maana Waziri wa Kilimo alitangaza yangeweza kukamilika Machi 31 lakini haikuwezekana - Vyama vya msingi AMCOS nao wanafanya ‘fojari’ wanaandika majina ambayo hayapo. Nataka Polisi wawashughulikie hawa!

Uamuzi wa Serikali kununua hizi korosho sio inafanya biashara, ni kawaida kwa Serikali iliyo makini kuangalia shida za Wananchi wake. Enzi za Rais Mstaafu Kikwete ukame ulitokea Loliondo wafugaji walipewa ng'ombe bure walionunuliwa na Serikali

Hadi leo Wakulima wa Korosho wamelipwa Sh. Bilioni 578.7, Usafiri Bilioni 5.1, Magunia Milioni 6.4, AMCOS Sh. Bilioni 3, Vyama vya Ushirika vimelipwa Milioni 670. Waendesha maghala wamelipwa Sh. Bilioni 6.6 na Uratibu wamelipwa Bilioni 1.3

Chanzo: JamiiForums

Loading...

No comments: