RAISI MAGUFULI AITAKA TANESCO KUREJESHA MILLIONI 27 ZA MWEKEZAJI MTWARARaisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amelitaka shirika la Umeme nchini (Tanesco) kumlipa Tsh Milion 27 mwekezaji wa kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Mtwara vijijini. 

Mara baada ya kutompa ushirikiano wa kumfikishia umeme kwenye kiwanda hicho, Tanesco ilimtaka mteja huyo kujinunulia Transformer kitendo ambacho Mheshimiwa Rais Magufuli kakipinga kwa kusema "Haiwezekani anunue transformer alafu mje kumlipisha bili tena". 

Mheshimiwa Raisi amewataka watendaji wake kama hawawezi kuwatumikia wananchi ni heri waondoke wakafanye shughuli nyingine kuliko kuwatesa wananchi. 

Post a Comment

0 Comments