RIHANNA AZIDI KUJIONGEZEA BIASHARA, SASA NI KWENYE VIPODOZI...

Rihanna Fenty beauty

Msanii wa miondoko ya RnB, Rihanna ameingia rasmi kwenye biashara ya vipodozi na bidhaa za ngozi mwaka huu huku akiisajili kibiashara kampuni yake kwa jina la FENTY SKIN. 

Rihanna amefikia uamuzi huo baada ya kampuni yake ya mavazi FENTY BEAUTY kuwa ikifanya vizuri kwa kuingiza sokoni bidhaa kama Make Ups, Miwani, viatu na mavazi mbali mbali yanayowavutia sana mashabiki wake. 

Mrembo huyo kwa sasa yupo tayari kuwaletea mashabiki wake mafuta ya ngozi na bidhaa nyingine kwa ajili ya ngozi zao. 

Kwa mujibu wa Bernard Arnault, ambaye ni mwenyekiti na Mkurugenzi wa kampuni hiyo aliweka wazi kuwa mauzo ya bidhaa za FENTY BEAUTY yalifikia kiasi cha Tsh. Trilioni 1.3 hadi ilipofika mwaka 2018. 

Post a Comment

0 Comments