RIPOTI YA CAG: MAZITO YALIYOIBULIWA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 10, 2019

RIPOTI YA CAG: MAZITO YALIYOIBULIWA

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Assad, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, wakati  akitoa ripoti za ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2018 ameibua yafuatayo;CAG Profesa Mussa Assad amesema Chadema kilinunua gari aina ya Nissan Patrol kwa Dola 63,720 sawa na Sh147.76 milioni ambalo lilisajiliwa kwa jina la mwanachama badala ya bodi ya wadhamini ya chama hicho.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema ununuzi wa BVR uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilibaini NEC ilinunua mashine 8,000 na kati ya hizo  5,000 hazikukidhi vigezo vya mkataba.

CAG Profesa Mussa Assad amesema Serikali ilikuwa ichagie Sh118 bilioni katika miradi 10 ambayo  ina ubia na washirika wa maendeleo lakini imetoa Sh7.3bilioni sawa na asilimia 6 na kusababisha Sh111bilioni kutopelekwa kinyume na makubaliano.

CAG Profesa Mussa amesema mashirika ya umma 14  ikiwemo Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na Benki ya TWB yana matatizo ya kifedha na kusababisha kuwa na madeni makubwa kuliko mtaji wake, kati ya mashirika hayo, 11 yana ukwasi hasi na mengine kujiendesha kihasara kwa miaka miwili.

Profesa Mussa Assad amesema kulingana na taratibu za ukaguzi wataendelea kutumia neno ‘dhaifu’, ametoa kauli hiyo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ripoti ya ukaguzi ya mwaka unaoishia Juni 2018 ambayo ina neno dhaifu katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi.

“Aidha nilibaini kuwapo kwa tatizo la uendelevu wa biashara katika kampuni ya uchapishaji ya Uhuru inayomilikiwa na CCM. Pia hati ya ardhi za nyumba 199 zinazomilikiwa na CCM Zanzibar zilionekana hazijasajiliwa kwa jina la bodi ya wadhamini bali zimesajiliwa kwa majina ya maofisa wa chama,” amesema.

“Kati ya mashirika hayo, 11 yana ukwasi hasi kwa maana yanajiendesha kwa hasara kwa zaidi ya miaka miwili sasa”

“Kufuatia hali hi, ni dhahiri kuwa mashirika hayo hayawezi kujiendesha bila kutegemea msaada kutoka Serikali kuu, hivyo ipo hatari ya kushindwa kuendelea kutoa huduma kwa jamii,” amesema Profesa Assad.
Loading...

No comments: