HATA MIMI NAYAJUA MAHABA - ROSA REE

Msanii wa Rap Bongo, Rosa Ree, amesema aliamua kuonyesha malavidavi kwenye nyimbo yake mpya ya 'Asante baba' ili kuwaonyesha mashabiki zake kwamba hata yeye anayajua mapenzi na sio mgumu kama watu wanavyomfikiria.Akizungumza na eNewz, Rosa Ree amesema haoni tatizo lolote kwa yeye kutambulika zaidi Kenya kimuziki kuliko Tanzania kwa kuwa anaamini nafasi yake hapa Tanzania itabakia palepale na kwa sasa anafurahia kwamba anaitambulisha vizuri nchi yake na hana hofu nafasi yake Tanzania itakuchukuliwa na Rapa Frida Aman.
Hata hivyo rapa Timmy Tdat wa Kenya naye hakusita kumsifia Rosa Ree na kusema, "hakuna mwanaume mzuri ambaye amekalika na hachezi michezo michafu ataacha kutamani kuwa na mpenzi kama Rosa Ree kwa kuwa ni mwanamke mwenye rangi nzuri, sura yake inavutia na ana mbwembwe ambazo ukiaa naye karibu huchoki kumuangalia, hivyo kwa sasa tunafanya kazi lakini kama mengine yakitokea itakuwa sio mbaya ni kama ajali kazini".
Pia Rosa Ree amemalizia kwa kusema kwa sasa hawezi kuwasaidia chochote wasanii wenzake waliotoka naye katika lebo ya 'The Industry' kwa kuwa yeye mwenyewe anajiona bado hajafikia kule anapopataka na anachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha anasukuma muziki wake ufike kule ambapo amelenga na akishafanikisha hilo atawasaidia wezake lakini pia anaamini wezake huko waliko wanafanya vizuri kwa kile wanachokifanya.

Post a Comment

0 Comments