RPC MUROTO: WATAKAOANDAMANA WATAPIGWA HADI KUCHAKAA

Raia watakaondamana kwa lengo la kuwashinikiza wabunge kushirikiana na Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG nchini Tanzania watakiona cha mtema kuni.Onyo hilo limetoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ambaye amewatahadharisha waliopanga maandamano hayo hapo siku ya Jumanne kwamba watapigwa hadi ''kuchakaa''.


Afisa huyo amesema kwamba baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo wamepanga kufanya maandamano kesho kulishinikiza Bunge kufuta kauli yake ya kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad.

Muroto ameonya kuwa wale wanaopanaga kufanya safari kuelekea mjini Dodoma ili kushiriki katika maandamano hayo wataambulia kupigwa na kuchakaa.

''Wale wote waliopanga kufanya maandamano mnamo Aprili 9, 2019 wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa," amesema Muroto.

Afisa huyo amesisitiza kuwa maswala ya bunge hutekelezwa ndani ya bunge na wala sio nje hivyobasi akawaomba wananchi wa Dodoma kuendelea na kazi zao kama kawaida kwani hakuna maandamano yoyote yatakayofanyika.

Ameongezea kuwa jeshi la polisi limejipanga kukabiliana na wale wote watakaoshirki katika maandamano hayo

Post a Comment

0 Comments