RUKSA KUSAJILI LAINI ZAIDI YA MOJA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 23, 2019

RUKSA KUSAJILI LAINI ZAIDI YA MOJA

Kupitia Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye serikali imetoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya laini za simu kuwa hakuna zuio la kutumia laini zaidi ya moja.Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rombo (Chadema) Joseph Selasini leo Jumanne Aprili 23, 2019 aliyetaka kujua kuhusu uvumi kwamba usajili mpya wa laini za simu unamtaka kila Mtanzania kumiliki laini moja.

Mbunge Selasini amehoji kuwa, "Waziri amesema Mei 1, utaanza usajili wa laini za simu kwa alama za vidole, akasema hakuna kumiliki laini 2 mpaka uruhusiwe, haudhani mtawatesa wananchi kwa maeneo ambayo mitandao mingine haipatikani?".

Akijibu swali hilo ndani ya Bunge Naibu Waziri amesema kuwa, "nilichosema ninatamani kila mtanzania awe na laini moja kwaa kila mtandao, akitaka laini nyingine aseme tu, tunaepuka utitiri wa laini nyingi, mfano ' Zile laini za tuma kwa namba hii ni laini zisizo na tija'.

Amesema kikubwa kinachoangaliwa ni kuona kama Serikali inaweza kupunguza utitiri ikiwemo baadhi ya watu kuwa na laini zaidi ya moja katika mtandao mmoja lakini kuwa na mitandao mingine haina shida.

Naibu Waziri huyo amesema kwamba utaratibu wa kusajili laini hautakuwa na madhara badala yake usalama zaidi ndio unaoangaliwa.

No comments: