RUMMENIGGE KUSTAAFU UTENDAJI UKUU BAYERN MUNICH, OLIVER KAHN KURITHI MIKOBA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 9, 2019

RUMMENIGGE KUSTAAFU UTENDAJI UKUU BAYERN MUNICH, OLIVER KAHN KURITHI MIKOBA


Mtendaji Mkuu wa klabu ya FC Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha kwamba ana mpango wa kustaafu kuitumikia klabu hiyo mwishoni mwa msimu wa 2020/2021. 

"Nafikiri ni muda sahihi wa kung'atuka. Nimekuwa nikifanya hivi kwa miaka 20 sasa." Alisema Karl Heinz ambaye katika ujana wake aliichezea klabu hiyo na kushinda taji moja la dunia, mawili ya Ulaya, makombe mawili ya Bundesliga na mawili ya michuano ya ndani. 

Rummenigge pia amedokeza kwamba Bayern Munich wana mpango wa kumteua nahodha wa zamani wa klabu hiyo Golikipa Oliver Kahn kuwa mrithi wake. 
Loading...

No comments: