SANTIAGO ASCACIBAR APIGWA MARUFUKU KUJIHUSISHA NA MICHEZO KWA WIKI SITA

Kiungo Santiago Ascacibar (mwenye jezi nyeupe) akipewa kadi nyekundu 

Kiungo raia wa Argentina anayekipiga katika klabu ya VFB Stuttgart ya Ujerumani Santiago Ascacibar amepigwa marufuku ya wiki sita kushiriki shughuli zozote za kimichezo ikiwa ni baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtemea mate kiungo Kai Havertz wa Bayern Leverkusen katika mchezo uliopigwa mwishoni mwa juma.

Ascicabar alitakiwa akose mchezo mmoja tu unaofuata lakini bodi ya Ligi ya Bundesliga ilipokaa ikaamua kumlima adhabu zaidi kwa kitendo chake ambacho si cha kiungwana michezoni. 

Bayer Leverkusen walishinda 1-0 dhidi ya VFB Stuttgart goli likifungwa na Kai Havertz Dk 64 ya mchezo huku Santiago Ascacibar akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90 ya mchezo huo. 

Post a Comment

0 Comments