SERIKALI KUANZISHA SOKO LA MNADA WA MADINI WILAYANI HAI KILIMANJARO


Serikali Wilayani Hai imeamua kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyowaagiza wakuu wa mikoa kuanzisha masoko ya madini katika mikoa yao ili kurahisisha biashara ya madini nchini.

Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alisema kuwa wameamua kuanzisha mnada wa kuuza madini katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwakuwa ni eneo wanaloingilia na kutoka wageni wengi hivyo ni sehemu sahihi ya kutangaza madini yetu ya Tanzania kwa Wageni. 

Post a Comment

0 Comments