SERIKALI YATOA TAHADHARI YA UWAPO WA UGONJWA DENGUE

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto  imetoa tahadhari juu ya kuwapo kwa ugonjwa wa homa ya dengue nchini, huku Dar es Salaam ikiwa na wagonjwa zaidi ya 200 waliobainika.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto  Dk Faustine Ndugulile

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Jana, Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto  Dk Faustine Ndugulile amesema mikoa ya Dar es Salaam na Tanga imebainika kuwapo kwa wagonjwa wa homa hiyo. Hadi kufikia April 2, 2019 kati ya watu 470 waliopimwa, wagonjwa 307 wamethibitishhwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Dengue, na kati ya hao 252 ni kutoka Dar es salaam na 55 ni kutoka Tanga.

"Dalili za ugonjwa huo kuwa ni homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambikizwa  virusi vya ugonjwa huu", amesema Dkt. Ndugulile.

Ugonjwa wa homa ya Dengue unasababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu wa aina ya “Aedes” ambao ni weusi wenye madoadoa meupe yenye kung’aa, ambapo hawa huwa na tabia ya kuuma zaidi wakati wa mchana hasa wakati wa asubuhi jua linapochomoza na jioni jua linapozama.

Dk Ndugulile amewataka wananchi wa maeneo tajwa kuchukua tahadhari ikiwamo kufukia maji na kujikinga na mbu.

Post a Comment

0 Comments