SHABIKI SIMBA ALIYETEMBEA KWA MGUU ATUA MTAA WA MSIMBAZI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, April 6, 2019

SHABIKI SIMBA ALIYETEMBEA KWA MGUU ATUA MTAA WA MSIMBAZI

Shabiki wa timu ya Simba aliyetembea kwa mguu kutoka Mbeya mpaka Dar es Salaam, Ramadhan Salum Mohamed amepokelewa kishujaa kishujaa na mashabiki wenzake mitaa ya Msimbazi ambako ndio makao makuu ya klabu ya Simba, na kumuahidi kumrudisha kwa ndege."Nimetumia siku 10 kutembea tangu 26 machi mpaka Aprili 24, kikubwa ilikuwa nikuja Dar kwa mguu kurudi ningedandia hata lori. "Mikumi niliombewa lifti na maskari ili kunivusha eneo la wanyama kwani kila hatua nilikuwa nafuata sheria za nchini, " Ramadhan Salum Mohamed alieleza.

Amesema anamuomba Mungu Simba ishinde dhidi ya TP Mazembe ili kumtia moyo kwa kile alichokifanya kwa kutembea kwa mguu baada ya hapo ana mpango wa kupanda mlima Kilimanjaro.

"Dhamira yangu imetimia naipenda Simba hii nimerithi kutoka kwa baba yangu mzazi,wachezaji wajitume waelewe kwamba tunahitaji kuona wanafanya kazi yakufurahisha mashabiki" alimaliza.
Loading...

No comments: