SHAUKU YATANDA, MAPINDUZI YA KIJESHI SUDAN

Jeshi la Sudan limetangaza kuwa litatoa taarifa muhimu hivi karibuni, hali inayohisiwa kuwa utawala wa Rais Omar al-Bashir huenda ukafikia kikomo hivi karibuni.

Waandamanaji wameendelea kutaka Rais Bashir ang'oke madarakani

Wanajeshi wametanda katika makazi rasmi ya rais mapema asubuhi ya leo, shirika la Habari la kimataifa la AFP linaripoti.
Jeshi pia limezingira njia zote muhimu za kuingia na kutoka mji mkuu wa Khartoum.

Magari yaliyosheheni wanajeshi wenye silaha yameegeshwa kwenye barabara zote muhimu na madaraja kwenye mji mkuu, shirika la habari la Reuters linanukuu mashuhuda.

Matangazo ya kawaida ya redio ya serikali yamekatishwa na kwa sasa zinapigwa nyimbo za ukombozi.
Raia wanaimba jwa furaha, "serikali imeangushwa. Tumeshinda," shirika la Reauters linaripoti.

Maelfu ya watu wamo barabarani wakijaribu kuelekea makao makuu ya wizara ya ulinzi kuungana na waandamanaji ambao wamekuwa wakishinikiza rais Bashir kubwaga manyanga baada ya miaka 30 madarakani.

BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments