SHAVU LINGINE KWA PIERRE KONKI LIQUID, KUAMBATANA NA TAIFA STARS KWENDA MISRI

Msanii Peter Molel maarufu kama Konki Liquid 'Pierre' amepewa nafasi ya kuwenda kuishangilia timu ya taifa “Taifa Stars” nchini Misri kwenye michuano ya mataifa ya Afrika, AFCON 2019 itakayoanza mwezi juni 2019.

Pierre akifanya manjonjo yake kwenye picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika, Dk Tulia na waheshimiwa wengine.

Akingumza kwenye viwanja vya Bunge, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimueleza  Pierre Liquid kuwa atatafuta utaratubu Pierre awepo kwenye safari ya kwenda Misri kuishangilia Stars.

“Tutatafuta  utaratibu wakati Taifa Stars inakwenda Misri, na waheshimiwa wabunge tunakwenda Misri hatuwezi kukosa nafari moja ya ndege kwa ajili ya Pierre”-Waziri Mkuu aieleza.

Waziri mkuu pia alimtaka Pieree kuendelea kuwahamasisha watanzania kuishabikia stars.

Piere leo April 3, 2019 alilitembelea Bunge kwa mwaliko wa Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Post a Comment

0 Comments