SHILOLE AFUNGUKIA ISHU YA MIMBA

Staa wa Bongo Movie na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole” amezima tetesi za kutajwa kuwa ni mjamzito kutokana na unene alionao kwa sasa.Shilole alisema, kutokana na mwili wake kuwa mkubwa, watu wengi wanaamini kuwa ni mjamzito, kitu ambacho si kweli.

“Nadhani ni mabadiliko ya mwili tu, kwa sasa nimeongezeka, lakini hii haimaanishi kuwa ni mjamzito, kupata mtoto ni majaliwa na kama ni hivyo nitashukuru sana, lakini ninachofahamu kwa sasa mwili wangu umeongezeka na si vinginevyo,” alisema Shilole.

Aidha, Shilole alisema licha ya kutotamani kuongezeka kwa mwili wake, lakini mabadiliko hayo hayamletei kero yoyote na hawezi kujinyima kula kwa kuwa anaamini hiyo ni moja ya kuridhika na hali ya maisha aliyonayo.

Shilole ambaye ni mke wa Uchebe ni moja ya mastaa wapambanaji na miongoni mwa washindi wa tuzo ya Malkia wa Nguvu 2019 iliyoandaliwa na Clouds Media.


Post a Comment

0 Comments