SIMBA YAICHAPA MBAO, BOCCO, KAGERE WANG’ARA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, April 1, 2019

SIMBA YAICHAPA MBAO, BOCCO, KAGERE WANG’ARA

Timu ya Simba imeibuka na ushindi  mnono wa magoli 3-0 dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. Magoli mawili ya nahodha John Bocco dakika ya 25 na 59 (penati) na goli la mshambuliaji Meddie Kagere dakika 80 kwa njia ya mkwaju wa penati yalitosha kuwaangamiza Mbao FC.Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 57, ikiwa imecheza michezo 22 nafasi ya tatu ikipunguza tofauti ya pointi na vinara wa ligi hiyo timu ya Yanga yenye pointi 67, huku Azam ikiwa ya pili na pointi 59, zote zikiwa zimecheza micehzo 28.

Ushindi huo unaiweka Simba katika mazingira mazuri wakati ikijiandaa na mchezo wa kwanza kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe utaochezwa Jumamosi.


Loading...

No comments: