SIPENDI KUISHI MAISHA FEKI-SHILOLE

Staa wa Bongo Movie na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amesesema yeye sio kama mastaa wegine ambao wanaishi maisha ya kuigiza,  yeye anaishi maisha yake halisi na kujituma kwenye shuguli zake bila kiki.

Shilole na mume wake Uchebe
"Sipendi kuishi maisha feki, ndio maana unaona napambana kwa kadri ninavyoweza ili kutengeneza maisha yangu halisia, Shilole awe ni yuleyule mahali popote nitakapokutana na watu.

"Muda wangu naupangilia vizuri kufanya biashara ya chakula, muziki pia kumtunza mume wangu na ndio maana unaweza kukuta naisha naye kwa amani siku zote.

"Awali wengi walikuwa wanajaji kwa nini Shilole ameolewa na mtu ambaye sio maarufu, unajua ndoa ni kitu kikubwa, nilihitaji mtu ambaye ni mwelewa na mpambanaji ndivyo alivyo ninayeishi naye,"anasema.

Shilole anasema anaamini katika kujituma na kutumia fursa za nafasi aliopo kwamba ndivyo vinavyomfanya maisha yake yastawi kila siku.

Post a Comment

0 Comments