SPIKA ATAJA DENI LA MBUNGE LEMA, KUHOJIWA NA KAMATI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 3, 2019

SPIKA ATAJA DENI LA MBUNGE LEMA, KUHOJIWA NA KAMATI


Leo Aprili 3,Kwenye kiako cha Bunge,baada ya kipindi cha maswali namajibu,  Spika wa Bunge, Job Ndugai ametaja deni analodaiwa Bunge Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema)Godbless Lema kuwa ni zaidi ya shilingi milioni mia nne kitu ambacho spika amendai huenda deni hilo linamsabishia  msongo wa mawazo mbunge huyo.


“Yapo mambo ambayo hawasemi wacha tuseme kidogo Mh Lema tangu aje hapa Bungeni amekopa Shilingi milioni 644…ameshalipalipa hivi sasa anadaiwa milioni 419 huu ni msongo wa mawazo ndio maana anafika mahali anajilipua tu na kadhalika,” Ndugai amesema.

Spika Ndugai aliyasema hayo wakati akiiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumhoji Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kuhusu uamuzi wake wa kuunga mkono kuwa Bunge ni dhaifu huku akianika hadharani madeni yake.

Spika Ndugai ametaka kamati hiyo kukutana saa 8.00 mchana leo na kwamba ikiwezekana  suala hilo  kesho liwe limekamilika.

“Kamati ya maadili saa 8.00 muanze kikao chenu na Lema saa 7.00 mchana uwe katika maeneo yale maana ulisema huogopi na mimi niwaambie waheshimiwa wabunge Spika Ndugai haogopi pia,”amesema.


Loading...

No comments: