SPIKA NDUGAI ATOLEA UFAFANUZI SAKATA LA CAG

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, leo mchana Alhamisi Aprili 4, 2019 akiiongoza kikao cha Bunge, ametoa ufafanuzi juu ya azimio la Bunge la kutokufanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuwa Bunge limeazimia kutofanya kazi na kutoshirikiana na CAG na sio ofisi ya CAG.“Hakuna wakati wowote ambao Bunge limekataa kufanya kazi na taasisi ambayo ni ofisi ya CAG. Bunge hili limekataa kufanya kazi na mtu anayeitwa Profesa Assad basi. Tusiripoti tofauti tukauchonganisha umma na kuuchanganya,” amesema Ndugai.

Aprili 2, 2019 Bunge lilipitisha azimio la kutofanya kazi na Profesa Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa Bunge ni dhaifu.


Post a Comment

0 Comments