SPIKA: TUNDU LISU AMESHALIPWA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, April 7, 2019

SPIKA: TUNDU LISU AMESHALIPWA

Ikiwa zimepita siku 10 tangu mnadhimu huyo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kumwandikia barua Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai akimtaka kumlipa mshahara na posho zake za kuanzia Januari, ndani ya siku 14 vinginevyo atashtaki mahakamani.Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema bunge limeshalipa madai  yote ya mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu huku akimwagiza kuwa kama ana jambo lolote kuwasiliana na mamlaka husika na si kutumia mitandao ya kijamii.

Akizungumza kwa njia ya simu  na gazeti la mwananchi,  Spika Ndugai alithibitisha wamba mbunge huyo ameshalipwa madai yake, Ndugai alisema,

“pale bungeni hatumuonei mtu hata kidogo labda nikate simu yako niangalie kama kweli amelipwa ninaweza kufanya kazi hiyo,” alisema Ndugai na baadaye kupiga simu na kueleza kuwa Mnadhimu huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni tayari ameshalipwa, “wameshamlipa,” alipoulizwa amelipwa madai gani alisema, “usitake tena… yaani hana madai. Kama ana madai mengine atasema.”Loading...

No comments: