WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA EAST AFRICA’S GOT TALENT

Baada ya kuzinduliwa jana jijini Nairobi , Waziri wa Michezo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amezindua tamasha kubwa la Vipaji Afrika Mashariki ‘East Africa’s Got Talent’ leo April 10, 2019 Serena Hotel, jijini Dar es Salaam.Usaili wa kwanza hapa Tanzania wa wasanii watakaoshiriki kwenye tamasha hilo kubwa unatarajiwa kufanyika Mei 21 mwaka huu kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere JNICC – Posta.

Aidha waziri Mwakyembe ameipongeza Clouds Media Group kwa kuwa mstari wa mbele kwenye ubunifu na uthubutu kwa kuwa tamasha hili ni kitu ambacho kilikosekana hapa nchini kwa muda mrefu.

‘’Nilidhani watu wengine ndio wameleta, kumbe wao ni wadhamini tu, niseme tena Clouds kwa mara nyingine tena mmetutoa kimasomaso, mtaona nitakavyotamba Bungeni” Alisema Waziri Mwakyembe.

“Kitu mlichokifanya Clouds mmefungulia vijana wenye vipaji vya ajabu, sio wote watakaoshinda lakini wengi watapata nafasi” Alisema Waziri Mwakyembe.

Post a Comment

0 Comments