TANZANIA YAANZA VIBAYA AFCON, YAPIGWA 5-4 NYUMBANI

Mechi ya ufunguzi ya michuano ya AFCON chini ya miaka 17 imemalizika kwenye Dimba la Taifa na wenyeji Tanzania wameanza vibaya kwa kupoteza pointi zote tatu mbele ya Nigeria.

Katika mchezo huo Serengeti imekubali kufungwa jumla ya mabao matano kwa manne.

Mabao ya Tanzania yamewekwa kimiani na Edmund aliyefunga mawili kwa njia ya penati, Kelvin John na Morice.

Wakati huo mabao ya wageni, Nigeria yamefungwa na Ubani aliyefunga mawili, Olatomi, Amoo na Ibraheem.Post a Comment

0 Comments