Tengenezeni hata divai na gongo mahususi ya korosho - Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiendelea na ziara yake mkoani Mtwara amesema kuwa anaunga mkono kile alichosikia ni kutengenezwa kwa juisi ya korosho

Ameeleza hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa barabara ya Mtwara ,Newala -Masasi Km 210 Sehemu ya Mtwara -Mnivata Km 50.

“Nimeambiwa mnafanya utafiti wa kutengeneza juisi kutoka kwenye korosho, kama ni divai ya korosho itengenezwe,kama ni gongo ambayo ni spesho itengenezeni iliyopimwa, kwasababu hata hizi pombe kali nazo si gongo sema imepimwa... anayetaka kulewa kwa dakika mbili alewe," amesema Rais Magufuli

Amendelea kwa kusema, 'Huwezi serikali ikanunua korosho kwa kilo 3500 halafu ianze kulipia tena kodi kwenye Halmashauri ambayo ilishindwa kununua korosho,kwa hiyo hakuna ushuru wa Halmashauri ,hata senti tano hampati, mkitaka ushuru simamieni vizuri'. 

Post a Comment

0 Comments