TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE: BALE, RODRI, SESSEGNON, TRIPPIER, MUSTAFI, VIDAL, CAMACHO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 23, 2019

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE: BALE, RODRI, SESSEGNON, TRIPPIER, MUSTAFI, VIDAL, CAMACHO

Real Madrid wanaangalia uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wa kimataifa kutoka Wales Gareth Bale msimu ujao - au wamtoe mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29- kwa mkopo ikiwa hawatampata mnunuzi anayefaa. (Marca)Bale anaweza kujiunga na Manchester United kwa mkataba wa deni mdogo ambapo anaweza kulipwa £5m. (Marca, via Mirror)

Manchester City wako tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya £60m ili wasaini mkataba na Rodri, ambaye yuko katika kiwango cha juuzaidi cha soka. Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Uhispania mwenye umri wa miaka 22- kutoka timu ya from Atletico Madrid kama mchezaji wa kiungo cha kati anayeweza kujaza nafasi ya Mbrazili Fernandinho, mwenye umri wa miaka 33. (Telegraph)

Juventus wako tayari kuichagiza Tottenham msimu ujao kwa kumchukua Ryan Sessegnon mwenye umri wa miaka 18 anayechezewa Fulham' safu ya nyuma kushoto. (Express)

Tottenham wamejiandaa kumuuza mchezaji wa safu ya nyuma wa timu ya England Kieran Trippier msimu ujao, huku Manchester United na Napoli wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka b28. (Sun)

Unai Emery atasaini mkataba na Arsenal msimu huu - huku mlinzi wa kimataifa Mjerumani Shkodran Mustafi, mwenye umri wa miaka 27, akiwa miongoni mwa wachezaji wanaouzwa . (mail)

Barcelona wanatarajia kumtoa mchezaji wa safu ya kati wa kimataifa wa kutoka Chile Arturo Vidal, mwenye umri wa miaka 31, kwa kurefusha mkataba wake wa sasa , utakaokamilika 2021. (Sport)

Wolves na Sporting Lisbon ya ureno wanataka kusaini mkataba unaoweza kubadilika na mchezaji wa Liverpool Rafael Camacho mwenye umri w amiaka 19. (Birmingham Mail)

Manchester United wametoa ombi la €60m (£51.9m) kwa Bayern Munich wakiomba wasaini mkataba na Niklas Sule, mwenye umri wa miaka 23 kwa msimu unaokuja . (Sport 1, via Teamtalk)

Mchezaji wa zamani wa Manchester City safu ya kati Yaya Toure, mwenye umri wa miaka 35, yuko tayari kuhamia katika Ligi kuu za soka nchini Marekani au kujiunga na timu ya Asia. (Goal)

Manchester United wanatarajia kutengeneza faida ya £50m kutokana na kampeni zao za Ligi kuu ya Championi ,licha ya kuchujwa na Barcelona katika mechi ya robo fainali. (Sun)

Meneja wa zamani wa Manchester United David Moyes haamini kuwa timu hiyo itamalika miongoni mwa timu nne bora msimu huu. (Sun)

Meneja Nigel Adkins anasema ataketi chini na makamu mwenyekiti Ehab Allam siku ya Alhamisi ili kufahamu wazi mipango ya Hull City' kwa msimu ujao . (Hull Daily Mail)

Mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 27, ameiambia Manchester United kwamba wanahitaji 'kusaidia 'katika mchezo wao katika Old Trafford. (Express)

meneja wa zamani wa timu za taifa za Ujerumani na Marekani Germany Jurgen Klinsmann amekanusha tetesi kwamba atakuwa meneja wa Hertha Berlin (Goal)

No comments: