TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE: OBLAK, DE GEA, FERDINAND, FRASER, ODEGAARD, CAVANI

Paris St-Germain inafikiria kumnunua kipa wa Manchester United davdi De Gea kwa dau la £90m huku kipa huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 akitarajiwa kulipwa £450,000 kwa wiki na mabingwa hao wa Ufaransa. (Star)Manchester United inajiandaa kumnunua kipa wa Atletico Madrid mwenye umri wa miaka 26 Jan OBlack. (ESPN)


Mchezaji wa zamani wa Man United na Uingereza Rio Ferdinand amekutana na naibu afisa mkuu mtendaji Ed Woodward ili kuzungumzia kuhusu kuwa mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo (Mail)

Winga wa Bournemouth na Uskochi Ryan Fraser, 25, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu kwa kuwa anataka kujiunga na klabu ya juu (Mirror)


Real Madrid wako tayari kumuacha kiungo wa kati wa Norway mwenye umri wa miaka 20 Martin Odegaard ajiunge na Ajax kwa mkopo wa miaka miwili. (Mail)


Chelsea na Manchester United wanachunguza hali ya mshambuliaji wa PSG na Uruguay mwenye umri wa miaka 32 Edinson Cavani, ambaye anataka kujiunga na ligi ya Uingereza.(Calciomercato)
Liverpool inajiandaa kumpatia Alex Oxlade-Chamberlain kandarasi mpya hadi 2023 - siku chache tu baada kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25 kurudi baada ya jeraha la muda mrefu. (Mirror)


Inter Milan inaendelea na mazungumzo ya kutaka kumsaini beki wa Brazil Danilo, 27, kwa dau la £18m kutoka Manchester City. (Mail)

Wolves watajaribu tena kumsaini beki wa Sweden mwenye umri wa miaka 24 Victor Lindelof kutoka Manchester United, baada ya kufeli kumsaini mwisho wa msimu uliopita. (Teamtalk)


Beki wa Ajax na Uingereza Matthijs de Ligt, 19, anatabiri kwamba huenda asigharimu zaidi ya dau alilonunuliwa mchezaji mwenza Frenkie de Jong, aliyenunuliwa na Barcelona kwa dau la £65m, huku uvumi unaozunguka hatma yake ukiendelea.. (Mirror)


Beki wa kulia wa klabu ya Nice na Algeria Youcef Atal, 22, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Chelsea mwisho wa msimu huu iwapo Fifa itaondoa marufuku ya uhamisho wa klabu hiyo. (Telegraph)


Real Madrid imefanya mazungumzo na klabu ya Lyon kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Tanguy Ndombele. (AS)

eki wa West Ham, 20, na Uingereza Reece Oxford anakaribia kuandikisha mktaba wa kudumu na klabu ya Bundesliga Augsburg kwa thamani ya £8m. (Sky Sports)


Wachezaji wa Arsenal wameshangazwa na mbinu anazotumia kocha wao mpya Unai Emery wakati wa msururu wa matokeo mabaya wa klabu hiyo. (Telegraph)


Mshambuliaji wa Barcelona na Ghana Kevin-Prince Boateng, 32, anasema kuwa angeichezea Man United kwa miaka 10 iwapo angepata motisha (Goal)


Beki wa Brazil Dani Alves, 35, anafikiria hatma yake katika klabu ya Paris St-Germain kufuatia kufungwa na klabu ya Rennes katika fainali ya kombe la Ufaransa. (RMC)

Kipa wa Barcelona na Uholanzi Jasper Cillessen, 30, amethibitisha kwamba ataondoka katika katika klabu hiyo ya Uhispania ili kushiriki mechi nyingi (Marca)


Kipa wa Manchester United Dean Henderson - ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Sheffield United - anatarajiwa kuanza mazungumzo kuhusu hatma yake ya Old Trafford lakini atataka kusalia katika uwanja wa Bramall Lane msimu ujao. (Express)

Post a Comment

0 Comments