TETESI ZA USAJILI: HAKIM ZIYECH WA AJAX AVIVUTIA VIGOGO WA EPL NA BUNDESLIGA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, April 23, 2019

TETESI ZA USAJILI: HAKIM ZIYECH WA AJAX AVIVUTIA VIGOGO WA EPL NA BUNDESLIGANyota wa klabu ya Ajax, Hakim Ziyech amevivutia vilabu vingi vikubwa barani Ulaya baada ya kuonesha kandanda safi kabisa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (Champions League). 

Sasa gazeti la Daily Mirror limeripoti kuwa klabu ya Liverpool nao wamejiunga kwenye mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo. 

Kabla ya hapo, ni vilabu vya Manchester City, Arsenal, Manchester United na Bayern Munich ndio walikuwa wanahusishwa na kutaka kunasa saini ya kiungo huyo wa kimataifa wa Morocco ambaye anapatikana kwa dau dogo la Pauni Milioni 25 tu. 

Sasa nani ataweza kukamilisha kumsajili? Ngoja tusubirie. 
Loading...

No comments: