TETESI ZA USAJILI: RABIOT KUIKACHA LIVERPOOL, KUIKUBALIA REAL MADRID - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, April 3, 2019

TETESI ZA USAJILI: RABIOT KUIKACHA LIVERPOOL, KUIKUBALIA REAL MADRIDTetesi za soka leo hii zinasema kuwa kiungo wa PSG, Adrien Rabiot anatarajiwa kuikataa klabu ya Liverpool na kujiunga Real Madrid majira ya kiangazi kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Marca la nchini Hispania. 

Kinachoipa nguvu hii habari ni kuwepo kwa gazeti jingine la CalcioMercarto ambalo nalo limeripoti kwamba Mfaransa huyo atakataa ofa ya Liverpool ili kutua Bernabeu pindi mkataba wake ukifikia tamati mwezi Juni ndani ya PSG. 

Rabiot amekataa kusaini mkataba mpya PSG kutokana na kutopewa uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Thomas Tuchel na ameripotiwa kuchagua kujiunga na Real Madrid kwasababu ya kuvutiwa na kocha Zinedine Zidane. 

Loading...

No comments: