TETESI ZA USAJILI: THORGAN HAZARD MGUU MMOJA DORTMUND, MMOJA LIVERPOOL

Thorgan

Winga Thorgan Hazard amewaarifu klabu ya Borussia Dortmund anataka kujiunga nao mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa taarifa kutoka KICKER.

Dortmund wanajiandaa kuwalipa Borussia Monchengladbach kiasi cha Pauni Milioni 35 kwa winga huyo wa kimataifa wa Ubeligiji ambaye mkataba wake unafikia tamati mnamo mwaka 2020. 

Wakati hayo yakiendelea, timu yake Thorgan, Borussia Monchengladbach, wangependa kumuuza Thorgan Hazard kwa klabu iliyo nje ya Bundesliga, kwa mujibu wa taarifa kutoka Het Nieuwsblad. 

Vinara wa Ligi kuu ya Uingereza (Liverpool) wapo tayari kutoa kiasi cha Pauni Milioni 40, ambazo ni Milioni tano zaidi ya ile ofa ya Dortmund ili kufanikiwa kumnasa mbeligiji huyo majira ya kiangazi. 

Post a Comment

0 Comments